Tuesday, December 11, 2007

Marafiki wakubwa


Tom Cruise na Will Smith wakiwa katika sherehe ya ufunguzi wa picha mpya ya Will inayoitwa "I am the Legend" katika theatre ya wachina kule Hollywood.Thats what friend are!

Is he really gay?



Ladies....why all goodlooking guys are taken by men? What is going on in the world. Are men afraid of women?
Watch him on his CNN program 360.I am so disappointed if it's true.

Tuesday, December 4, 2007

Wapenzi wapyaa


Super model wa kiingereza Naomi Campbell anaonekana na mpenzi mpya kabisa (jina kapuni).

Xtina avua nguo


Mwanamuziki mpendwa Christina Aguilera amepozi uchi wa mnyama kutuonyesha mimba yake.Utapata habari zaidi za picha hiyo katika toleo lijalo la gazeti la Claire hapa USA.

Thursday, November 29, 2007

Sunday, November 18, 2007

Tatizo lake nini


Pamoja na hela zote alizonazo anashindwa kujipatia mwanamke mzuri anahangika na watoto,hivi sasa R kelly ana makosa 14 ya ubakaji wa watoto.

Friday, November 9, 2007

Hatimae J-Lo ni mjamzito


She finally admit her pregnancy with hubby Mark Anthony. Cant wait to see that little one.

Thursday, November 8, 2007

Is she another gold digger


Getting divorce means getting money.Here is Shaq with his estrange wife.The court will finalize.

Saturday, November 3, 2007

Kumetokea nini Dennis?


Mchezaji maarufu wa zamani wa basketi nchini Marekani Dennis Rodman anaonekana hivi siku hizi.

Thursday, November 1, 2007

Ice T na Coco

Ice T na mkewe Coco wakionekana kusheherekea siku ya halloween.Hii ni sikukuu ya wachawi lakini sasa imegeuka kuwa na maana mbalimbali marekani.

More halloween


Christina Aguilera na Mumewe

Tuesday, October 23, 2007

They wanna!


Baaada ya kuolewa,kuzaa,kuhamia Marekani nk ....Spice girls wamerudi tena ulingoni na vitu vipya.

Thursday, October 18, 2007

Obama na binamu yake


Makamu wa Raisi nchini Marekani mzee Dick Cheney anasemakana kuwa ni binamu wa mbali wa mgombea mweusi wa kiti cha Urais nchini Marekani senator Barack Obama.Hayo ni matokeo ya DNA yanayoendelea nchini hapa kutafuta nani katokea wapi sababu kila mtu ni mzamiaji nchi hii.Obama akishinda uraisi atakuwa mwafrika wa kwanza kushika kiti hicho cha juu kabisa duniani wakati binamu yake atakuwa ni mwafrika(mzungu) wa kwanza kutwaa madaraka ya umakamu wa raisi wa marekani.
Do the maths!

Nini kinaendelea


Huyu mwanadada anasemekana kuwa mzuri kuliko wanawake wote duniani sasa sijui alikua anafikiria nini alipoamua kuvaa hivyo na kutoka?
Mrs Douptfire shoes

Wednesday, October 3, 2007

Britney anyang'anywa watoto wake


Mahakama nchini Marekani imeamua kumnyan'ganya Britney Spears watoto wake wawili na kumkabidhi kwa baba yao Kevin Fedeline,Britney kashindwa katika kesi iliyokua inaendelea muda sasa kutokana na tabia zake za ajabu anazozionyesha siku za karibuni.

Tuesday, October 2, 2007

Thursday, September 27, 2007

Wednesday, September 19, 2007

Wazee wa Macharanga!?


Kanye West aliungana na Diddy, Jay-Z na producer LA Reid katika sherehe ya kuadhimisha miaka 50 ya kuzaliwa kwa gazeti la GQ iliyofanyika jumanne(jana) Newyork.

Tuesday, September 18, 2007

Rosie amtolea nje Oprah


Kuna usemi nchini Marekani kuwa Oprah akikuita haukatai,lakini safari hii Oprah kakumbana na kukataliwa pale alipomwalika mtangazaji Rosie Odonnell katika kipindi chake ambapo alitaka wazungumzie kuhusu kitabu kipya cha Rosie kinaitwa "Celebrity Detox".Rosie anayejulikana kwa kukosoa watu na hasa wale wanaojulikana pamoja na kuropoka mambo mengi bila mpangilio, alimtumia ujumbe Oprah akimueleza hataweza kuhudhuria mwaliko labda siku nyingine.Bahati mbaya Oprah anakualika mara moja tu.
DEAL WITH IT BIG O

Friday, September 14, 2007

K-Fedeline kupokea dola 20,000 kila mwezi


Mahakama nchini marekani imeamua kuwa Britney Spears atakuwa anamlipa aliyekuwa mumewe na baba wa watoto wake wawili Kevin Fedelina dola elfu ishirini kila mwezi kwa maisha yake yote ikiwa ile wamarekani wanaita "Spouse support" .Hayo ni makubaliano yaliyopo ili kumzima moto asiendelee kugombania watoto kutoka kwa Britney.
What a bastard?

Thursday, September 13, 2007

Mlinzi wa fasheni anahitajika



Blog hii inatafuta mtu mjuzi wa mambo ya ulinzi na usalama anisaidie kuwatoza faini warembo wanaotuharibia mavazi yetu kama mwanadada huyu anayeitwa Cate Blanchett.Pamoja na filamu nyingi alizowahi kucheza,Cate anapatikana katika picha inaitwa "The Aviator" ya mwaka 2005 akiwa na Leonardo Dicaprio ambayo ilimpeleka nyumbani na tuzo kubwa la wacheza sinema Duniani la Oscar.Macho yanauma nikiliangalia hilo gunia alilovaa.

Wednesday, September 12, 2007

Du nimenenepa


Baada ya kushindwa kutumbuiza jukwaani katika matuzo ya MTV yanayotolewa kila mwaka kwa wanasanaa mbalimbali hapa nchini Marekani,Britney spears alilia sana nje ya ukumbi akidai amanenepa kama nguruwe.Britney ambaye miaka ya karibuni aliondoka ulingoni kutokana na majukumu ya kuzaa,alirudi upya kwa vituko vya kuvaa nguo fupi bila chupi ambapo tuliweza kujionea picha mbalimbali zikionyesha uchi wake.Watu walitarajia atarudisha umaarufu wake kwa kuteremsha shoo ya nguvu jukwaani lakini ilishiindikana.Washabiki wake wanataka asaidiwe ili arudishe vitu vyake tunavyovikosa.

Sunday, September 9, 2007

Like mom like daughter


Inakuwaje ukiwa mtoto wa Angelina Jolie?Pichani Zahara (Ethiopia) akiwa na mama yake huku wameshika pochi zinazofanana.

Monday, September 3, 2007

Diddy white party


Watu wengi wakiwa katika mapumziko ya sikukuu ya wafanyakazi hapa nchini Marekani,P Diddy alikua busy na kuandaa sherehe kubwa aliyoiita "white party" katika jumba lake kwenye visiwa vya Long jijini Newyork.Kila mwalikwa alitakiwa avae nguo nyeupe kama mnavyomuona Mariah Carey akiingia shehereni.
Bonyeza hiyo picha ili umwangalie kwa karibu.

Thursday, August 30, 2007

Mavazi ya wachunga ng'ombe yanapokua fasheni


Mwanamama Diane keaton ambaye licha ya kucheza filamu nyingi nzuri hii ni mojawapo naipenda sana inaitwa "Father of the Bride" alicheza kama mke wa Steve Martin.Angalia hiyo kofia,mkanda na mabuti...tayari kabisa kuungana na wamaasai porini.

Wednesday, August 29, 2007

Kwanini havai nguo za ndani?


Huyo anaonekana hapo ni bibie Britney Spears akiwa katika harakati zake mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutuonyesha vifaa vyake.

Monday, August 27, 2007

Separated at birth



Huyo ni binti maarufu sana katika katuni anaitwa Betty B akikubonyezea jicho moja.Hivi ni kweli nafanana nae?

Kipima pombe


Eve anaonekana akiwa amevaa kipima pombe mguuni.Ndivyo ambavyo mastaa wa hapa marekani wanajicheki na vipimo mbalimbali.
Leta lako mbongo.

Thursday, August 23, 2007

What if.....?


Wakati kampeni za kuwania uraisi zikiendelea Nchini hapa Marekani,mabinti nao hawapo nyuma kuwania nafasi za "ufirst lady".Pichani anaonekana binti ambaye anadai kuwa yeye ni Obama Girl akionyesha upande wake wa pili wa uzuri.Kumbuka Obama ni Mmarekani mweusi pekee kuwania nafasi hiyo ya juu sana duniani.
AM SURE YOU WON'T REJECT THIS SENATOR

Monday, August 20, 2007

Back to Basics


Rafiki yangu mpendwa (ni mkubwa sana kwangu) alinionyesha hili dude ambalo alikua anachezea alipokua mdogo,tunazungumzia zaidi ya miaka arobaini iliyopita.Sasa zimerudi tena,vipi ukimnunulia mtoto wako wa kiume zilizopendwa?
ROCK'EM SOCK'EM

Ellen na Portia


Mambo haya ni ya kawaida kabisa nchi hii,nasikia utamaduni huu unaingia kwa kasi sana bongo...
SOooooo IN HEART

Ndivyo wanavyojibadilisha


Huyu binti unayemuona hapa ni mwanaume.Amefanya kila kitu kujibadilisha kuwa mwanamke kasoro kitu kimoja....sehemu za siri.Kaka/dada huyu wa Australia anaonekana hapa akielekea Thailand kufanya operation itakayo muwezesha kuwa mwanamke kabisa.Katika passport yake alishindwa kujaza "gender" yake kama yeye ni mwanamke au mwanaume sababu yupo nusunusu bado.
Haya akina kaka kazi kwenu.

Wednesday, August 15, 2007

Mnamkumbuka George Michael


Mzee wa siku nyingi wa miziki mikali sana iliyovuma miaka ya tisini mwanzoni George Michael ameamuliwa na jaji kule nchini Uingereza kutumikia jamii kwa muda wa masaa 100 kutokana na kosa la kuendesha gari akiwa amelewa.George ambaye alijitangaza hadharani kuwa ni shoga atakuwa na kazi za kusafisha vyoo na barabara pale mjini London.
Hii sio mara ya kwanza kupewa adhabu za aina hiyo.Mwaka 1998,George alishawahi kutumikia jamii masaa 80 baada ya kukamatwa na polisi akiwa anafanya mambo yanayohusiana na ngono katika choo cha jamii pale Beverly Hills nchini Marekani

Tuesday, August 14, 2007

Mambo 10 ya Angelina Jolie



Inasemekana kuwa Angelina Jolie(32) ni mwanamke mzuri anayeishi,huyu dada ambaye ni mtoto wa mcheza sinema tajiri Jon Voight ana sifa na vituko nitakavyotaja hapa chini.
1.Alishinda Oscars toka katika picha inayoitwa "Lara Croft"
2.Ana kaka wa damu anayeitwa James ambaye waliwahi kula nae denda mbele ya mamilioni ya watu kule Hollywood.
3.Anakusanya visu vya kila aina kama hobby.
4.Ni balozi wa hiari wa Umoja wa Mataifa
5.Ana watoto wanne,watatu wa kuadopt na mmoja wa kumzaa.Watoto wake Maddox anatokea Cambodia,Pax anatokea Vietnam na Zahara anatokea Ethiopia.Mtoto wake Shiloh alizaliwa Namibia.
6.Anatembea na Brady Pitt ambaye anajulikana kama mwanaume mzuri anayeishi.
7.Licha ya kuwa na mahusiano ya muda mfupi na wanaume wengi aliowahi kucheza nao picha,dada huyo ana uhusiano wa mapenzi na mwanamke mmoja kwa kipindi cha miaka kumi.Amekiri majuzi kuwa toka aanze kutembea na Brady kaachana na yule mwanamke.
8.Alishawahi kuolewa mara mbili.
9.Yeye na baba yake hawaongei muda mrefu sana,jitihada za baba yake kutaka kusuruhisha ugomvi wao zimeshindikana.
10.Amekiri anataka kuongeza watoto wengi wa kuadopt wafikie 7 mpaka 14.

Friday, August 10, 2007

Hili ni vazi la wapi tena?



Huyo ni Victoria Beckham akienda kuhudhuria party mahali.
I DIDN'T KNOW LINGERIE TURNS OUT TO BE EVENING WEAR.ALL YOU HAVE TO DO IS GET YOUR CORSET AND THROW ON SOME MIN COAT....DONE! BUT WITH THOSE HIGH HEELS.......YOU REAL ARE..... "PRETTY WOMAN"

Thursday, August 9, 2007

Miaka 50 ya kuzaliwa na midomo ya miaka 10


Melanie Griffith asheherekea miaka 50 ya kuzaliwa japo midomo yake ina miaka 10.
MELANIE I WOULD LIKE TO VISIT WITH YOU FOR A MINUTE

Tuesday, August 7, 2007

Flavor Flav is always ontime


Flavor Flav kama anavyojulikana na washabiki wake alikua ni mmoja wa wanamuziki wa kundi la Public Enemy lililovuma miaka ya themanini kama sio tisini mwanzoni.Jamaa huyu anayejulikana kama PIMP(mtu anayetumia wanawake kutengeneza hela) na mwenye signature ya kuvaa saa shingoni kama unavyoona kwenye picha,alijizolea washabiki wengi aliporudi katika television akiwa na kipindi cha kutafuta mwanamke wa kuishi nae.Hapo nyuma hao ni baadhi ya mabinti waliokua wanamgombania.Flavor Flava alipata binti ambaye yupo nae baada ya kujaribisha kipindi hicho cha TV kilichojulikana kama Flavor of Love mara mbili kilichokuwa kinarushwa katika station ya VH1 nchini Marekani.Hivi sasa anarudi ulingoni na mapishi.
DON'T WORRY FLAV, I WILL BE ONTIME EVEN IF I DON'T HANG A WALL CLOCK ON MY NECK.

Monday, August 6, 2007

Pale binti yako anapokuwa mpinzani


Wakati sakata la kuwania urahisi nchini marekani likiwa linapamba moto kati ya vyama viwili maarufu nchini hapa,siasa imeingia ndani ya nyumba ya mmojawapo wa wagombea madaraka hayo ya juu kabisa duniani anayeitwa Rudy Giuliani.Mzee Giuliani ambaye alikua mayor wa mji wa NewYork na mgombea urahisi aliye mstari wa mbele kwa wapinzani wake wa chama cha Republican ameshitushwa na habari za bintie ambaye kaamua kujiunga na kambi ya ugombea urahisi ya Baraka Obama.Kumbuka Baraka ni mweusi wa chama cha Upinzani cha Democrat na ana asili ya kenya anaungwa mkono na binti huyo ambaye kaamua kusaliti baba yake.Habari hizo zilizopatika katika website ya myspace.com ilionyesha picha za binti huyo akiwa na rafiki zake na wakimuunga mkono Mr Obama.Mzee Giuliani alipoulizwa kutoa maoni yake alisema kwa kifupi anafurahi kitu chochote mtoto wake anachofanya.
PROUD PAPA

Diddy anavinjari na mtoto wa kiingereza



Mwanamuziki/ mfanyabiashara maarufu nchini marekani P Diddy anafanya mpango wa kupumzika katika boat lake na mtoto wa kiingereza ambaye ni mcheza sinema hapa marekani Sienna Miller.Kulikua na maongezi ya chini chini kwa muda mrefu kuhusu uhusiano wa Diddy na Miller ambao ulipekea Diddy kutengana na mama watoto wake Kim P. Mwanamke huyo ambaye kamzalia watoto mapacha Diddy aliamua kuondoka zake baada ya kuona boyfriend wake anahangaika na wazungu.Sasa hatuna habari rasmi za romance kati ya watu hao wawili lakini uwezekano ni mkubwa maana wote wawili ni mabachela wa kutupwa.
WE HEARD YOUR STORIES DIDDY,IS IT TRUE?