Wednesday, August 15, 2007

Mnamkumbuka George Michael


Mzee wa siku nyingi wa miziki mikali sana iliyovuma miaka ya tisini mwanzoni George Michael ameamuliwa na jaji kule nchini Uingereza kutumikia jamii kwa muda wa masaa 100 kutokana na kosa la kuendesha gari akiwa amelewa.George ambaye alijitangaza hadharani kuwa ni shoga atakuwa na kazi za kusafisha vyoo na barabara pale mjini London.
Hii sio mara ya kwanza kupewa adhabu za aina hiyo.Mwaka 1998,George alishawahi kutumikia jamii masaa 80 baada ya kukamatwa na polisi akiwa anafanya mambo yanayohusiana na ngono katika choo cha jamii pale Beverly Hills nchini Marekani

No comments:

Post a Comment

Please visit us oftenly.