Thursday, March 13, 2008

Rags to Riches


Pichani anaonekana mwanamke ambaye amesababisha Gavana wa jiji la Newyork(pichani chini) kujiuzuru kutokana na kashfa zilizomkumba za kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi na huyo malaya nje ya ndoa yake na vilevile kuvunja sheria za nchi.Wakati gavana Spitzer akiwa katika wakati mgumu kimaisha na kindoa mwanamke huyu anatengeneza mamilioni ya hela kwa kuuza nyimbo yake aliyoiweka katika ukurasa wake wa website ya "myspace" ambapo zaidi ya watu milioni moja wamenunua wimbo huo kwa kiasi cha dola 0.98.Msichana huyu wa miaka 22 alikua na wakati mgumu kimaisha na ikambidi ajiingize katika shughuli za kimalaya na kujiunga na danguro lililojulikana kama "Emperors Club vip"ambapo ndipo gavana alikua ni mteja wao.Hivi sasa danguro limefungwa na wanashikiliwa na polisi vilevile gavana alilazimishwa ajizuru.
Vyombo vya habari vinampatia ofa za hela nyingi msichana huyu iwapo atawaelezea hadithi yote kuhusu ile siku aliyolala na gavana.