Wednesday, August 15, 2007

Mnamkumbuka George Michael


Mzee wa siku nyingi wa miziki mikali sana iliyovuma miaka ya tisini mwanzoni George Michael ameamuliwa na jaji kule nchini Uingereza kutumikia jamii kwa muda wa masaa 100 kutokana na kosa la kuendesha gari akiwa amelewa.George ambaye alijitangaza hadharani kuwa ni shoga atakuwa na kazi za kusafisha vyoo na barabara pale mjini London.
Hii sio mara ya kwanza kupewa adhabu za aina hiyo.Mwaka 1998,George alishawahi kutumikia jamii masaa 80 baada ya kukamatwa na polisi akiwa anafanya mambo yanayohusiana na ngono katika choo cha jamii pale Beverly Hills nchini Marekani

Tuesday, August 14, 2007

Mambo 10 ya Angelina Jolie



Inasemekana kuwa Angelina Jolie(32) ni mwanamke mzuri anayeishi,huyu dada ambaye ni mtoto wa mcheza sinema tajiri Jon Voight ana sifa na vituko nitakavyotaja hapa chini.
1.Alishinda Oscars toka katika picha inayoitwa "Lara Croft"
2.Ana kaka wa damu anayeitwa James ambaye waliwahi kula nae denda mbele ya mamilioni ya watu kule Hollywood.
3.Anakusanya visu vya kila aina kama hobby.
4.Ni balozi wa hiari wa Umoja wa Mataifa
5.Ana watoto wanne,watatu wa kuadopt na mmoja wa kumzaa.Watoto wake Maddox anatokea Cambodia,Pax anatokea Vietnam na Zahara anatokea Ethiopia.Mtoto wake Shiloh alizaliwa Namibia.
6.Anatembea na Brady Pitt ambaye anajulikana kama mwanaume mzuri anayeishi.
7.Licha ya kuwa na mahusiano ya muda mfupi na wanaume wengi aliowahi kucheza nao picha,dada huyo ana uhusiano wa mapenzi na mwanamke mmoja kwa kipindi cha miaka kumi.Amekiri majuzi kuwa toka aanze kutembea na Brady kaachana na yule mwanamke.
8.Alishawahi kuolewa mara mbili.
9.Yeye na baba yake hawaongei muda mrefu sana,jitihada za baba yake kutaka kusuruhisha ugomvi wao zimeshindikana.
10.Amekiri anataka kuongeza watoto wengi wa kuadopt wafikie 7 mpaka 14.