Friday, September 14, 2007

K-Fedeline kupokea dola 20,000 kila mwezi


Mahakama nchini marekani imeamua kuwa Britney Spears atakuwa anamlipa aliyekuwa mumewe na baba wa watoto wake wawili Kevin Fedelina dola elfu ishirini kila mwezi kwa maisha yake yote ikiwa ile wamarekani wanaita "Spouse support" .Hayo ni makubaliano yaliyopo ili kumzima moto asiendelee kugombania watoto kutoka kwa Britney.
What a bastard?

Thursday, September 13, 2007

Mlinzi wa fasheni anahitajika



Blog hii inatafuta mtu mjuzi wa mambo ya ulinzi na usalama anisaidie kuwatoza faini warembo wanaotuharibia mavazi yetu kama mwanadada huyu anayeitwa Cate Blanchett.Pamoja na filamu nyingi alizowahi kucheza,Cate anapatikana katika picha inaitwa "The Aviator" ya mwaka 2005 akiwa na Leonardo Dicaprio ambayo ilimpeleka nyumbani na tuzo kubwa la wacheza sinema Duniani la Oscar.Macho yanauma nikiliangalia hilo gunia alilovaa.

Wednesday, September 12, 2007

Du nimenenepa


Baada ya kushindwa kutumbuiza jukwaani katika matuzo ya MTV yanayotolewa kila mwaka kwa wanasanaa mbalimbali hapa nchini Marekani,Britney spears alilia sana nje ya ukumbi akidai amanenepa kama nguruwe.Britney ambaye miaka ya karibuni aliondoka ulingoni kutokana na majukumu ya kuzaa,alirudi upya kwa vituko vya kuvaa nguo fupi bila chupi ambapo tuliweza kujionea picha mbalimbali zikionyesha uchi wake.Watu walitarajia atarudisha umaarufu wake kwa kuteremsha shoo ya nguvu jukwaani lakini ilishiindikana.Washabiki wake wanataka asaidiwe ili arudishe vitu vyake tunavyovikosa.

Sunday, September 9, 2007

Like mom like daughter


Inakuwaje ukiwa mtoto wa Angelina Jolie?Pichani Zahara (Ethiopia) akiwa na mama yake huku wameshika pochi zinazofanana.